Iraq

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
جمهورية العراق
Jumhūrīyat al-`Irāq
كۆماری عێراق
Komara `Îraqê

Jamhuri ya Iraq
Bendera ya Iraq Nembo ya Iraq
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Kiarabu: الله أكبر
(Allahu Akbar)
(Translation: "Mungu ni mkubwa")
Wimbo wa taifa: Mawtini (new);
Ardh Alforatain (previous)[1]
Lokeshen ya Iraq
Mji mkuu Baghdad[2]
33°20′ N 44°26′ E
Mji mkubwa nchini Baghdad
Lugha rasmi Kiarabu, Kikurdi[3]
Serikali Jamhuri, serikali ya kibunge
Jalal Talabani
Nouri al-Maliki
Uhuru
kutoka Dola la Uturuki
kutoka Uingereza

31 Oktoba 1919
3 Oktoba 1932
28 Juni 2004
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
438,317 km² (ya 58)
1.1
Idadi ya watu
 - 2005 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
28,807,000 (ya 40)
66/km² (ya 125)
Fedha Iraqi Dinar (IQD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+3)
(UTC+4)
Intaneti TLD .iq
Kodi ya simu +964

-

1 Wakurdi hutumiaEy Reqîb.
2 Arbil ni mju mkuu wa jimbo la kujitawala la Kurdistan.
3 Lugha rasmi za serikali kitaifa ni Kiarabu na Kikurdi. Kikurdi ni lugha rasmi ya jimbo la Kurdistan. Kikatiba lugha za Kiassiryani na Kiturkmeni ni lugha rasmi kieneo penye wasemaji wengi wa lugha hizi.


Ramani ya Iraq

Iraq ni nchi ya Asia ya Magharibi inayokaliwa hasa na Waarabu lakini pia n wengine. Inajumlisha eneo al Mesopotamia pamoja na sehemu ya jangwa la Shamu na ya milima ya Zagros. Imepakana na Kuwait, Saudia, Yordani, Syria, Uturuki na Uajemi. Kuna pwani fupi kwenye Ghuba ya Uajemi.

Iraq ni nchi yenye historia ndefu ilikuwa mahali pa miji ya kwanza ya dunia katika Sumeri na Babeli. Miaka ya nyuma imejulikana hasa kutokana na vita ya ghuba dhidi Marekani na nchi wenzake.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya Iraq ni jangwa lakini kuna eneo lenye rutba la Mesopotamia kati ya mito ya Frati na Hidekeli. Kaskazini ni hasa nchi ya milima inayopanda hadi ya kimo cha 3,611 m juu ya UB.

Hali ya hewa inalingana na mazingira. Kipindi cha kiangazi kuna joto kali. Majira ya Desemba-Februari kuna halijoto ya kupoa kwenye kusini na baridi kali mlimani.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Iraq ina akiba kubwa za mafuta ya petroli ardhini. Mapato kutokana na mafuta yalileta maendeleo makubwa nchini hadi mwanzo wa kipindi cha vita dhidi ya Uajemi chini ya serikali ya Saddam Hussein tangu 1981 kwanza, baadaye vita dhidi ya Kuwait na Marekani. Vita ya pili ya ghuba ya 2003 iliyoleta uvamizi wa Marekani ilizidi kuleta vifo na uharibifu. Vita hizi zimeharibu nchi pamoja na uchumi wake sana.

BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Iraq kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.