Nauru
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: "God's Will First" | |||||
Wimbo wa taifa: Nauru Bwiema | |||||
Mji mkuu | (hakuna) 1 | ||||
Mji mkubwa nchini | Yaren | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza , Kinauru | ||||
Serikali Rais
|
Jamhuri Baron Waqa | ||||
Uhuru kutoka ulinzi wa Australia, New Zealand, na Uingereza -kwa niaba ya UM |
31 Januari 1968 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
21 km² (ya 227) ‘‘(kidogo sana)’’ | ||||
Idadi ya watu - Julai 2011 kadirio - Msongamano wa watu |
9,378 (ya 216) 447/km² (ya 23) | ||||
Fedha | Dollar ya Australia (AUD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+12) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .nr | ||||
Kodi ya simu | +674
- |
Nauru ni nchi ya kisiwani ya Mikronesia katika Pasifiki ya kusini.
Ni nchi ndogo sana (ya tatu baada ya Vatikani na Monaco), yenye km² 21 pekee na wakazi wasiofikia 10,000.
Kisiwa jirani zaidi ni Banaba katika Kiribati chenye umbali wa km 300.
Nauru haina mji mkuu rasmi.
Historia[hariri | hariri chanzo]
Nauru imekaliwa na mchanganyiko wa watu kutoka Polynesia na Mikronesia tangu karne nyingi (miaka 3,000 hivi).
Katika karne ya 19 kisiwa kilitwaliwa na Ujerumani kama sehemu ya makoloni yake ya Pasifiki.
Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia kilikuwa eneo lindwa chini ya Umoja wa Mataifa (UM) na utawala ulikuwa mikononi mwa nchi tatu: Australia, New Zealand na Uingereza.
Watu[hariri | hariri chanzo]
Wakazi wengi (58%) ni wenyeji, wakifuatwa na watu kutoka visiwa vingine vya Pasifiki (26%), Wazungu (8%) na Wachina (8%).
Karibu wote (95%) ni wanene mno, hivyo hali ya afya si nzuri, hasa upande wa kisukari (40%).
Lugha[hariri | hariri chanzo]
Kuna lugha tatu tu ambazo huzungumzwa nchini Nauru: Kiingereza (lugha rasmi), Kinauru (lugha ya mawasiliano), na pijini inayounganisha Kiingereza, Kichina na Kiaustronesia.
Dini[hariri | hariri chanzo]
Wakazi wengi ni Wakristo (Waprotestanti na Wakatoliki kwa uwiano wa 2:1), wakifuatwa na wafuasi wa Bahai (10%) na Wabuddha (9%).
Uchumi[hariri | hariri chanzo]
Uchumi wa Nauru ulitegemea fosfeti iliyopatikana kisiwani kwa wingi. Kwa miaka kadhaa kisiwa kilikuwa nchi tajiri kabisa. Hadi mwaka 2001 huduma za hospitali zilikuwa bure, hapakuwa na kodi, na watu wengi walikuwa na magari mawili au matatu.
Tangu kumalizika kwa fosfeti hali ya kiuchumi imekuwa ngumu sana. 90% za wananchi wanakosa kazi. Serikali haina pesa za kutosha tena, huduma nyingi zimekwama, hata imeanza kupokea misaada kutoka Australia.
Angalia pia[hariri | hariri chanzo]
Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki |
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | Nyuzilandi | Niue | Pitcairn | Polynesia ya Kifaransa | Palau | Papua Guinea Mpya | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna |
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nauru kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|