Viparara (au Ndege-msumeno) ni ndege wa bahari wa jenasiRynchops, jenasi pekee ya familiaRynchopidae (Rhynchops na Rhynchopidae ni tahajia nyingine isio sahihi kwa mujibu wa uainishaji). Ndege hawa wanafanana na buabua lakini wana domo ambalo sehemu yake ya chini ni refu kuliko ile ya juu. Huruka kwa urefu mdogo juu ya maji wakiitia sehemu ya chini ya domo lao majini ili kuwakamata samaki wadogo. Jike huyataga mayai 3-6 kwa pwani za kanda za tropiki na za karibu na tropiki.