Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na kufungua akaunti. Angalia Wikipedia:Mwongozo ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.
wakati ugonjwa unazuru katika nchi ulipo, epuka kusalimu wengine kwa kushikana mikono
kaa nyumbani ukiwa mgonjwa (ugonjwa wowote - maana kinga yako ni dhaifu katika hali hii)
tembea na karatasi za shashi (kama huna, hata karatasi ya chooni / toilet paper) na uitumie ukikohoa au kupiga chafya, halafu uitupe mahali pa takataka
safisha mara kwa mara vitu unavyovigusa (vikiwa pamoja na kikombe, deski, simu yako)[1]; kama unayo, tumia dawa ya alikoholi (spirit – si konyagi!), lowesha karatasi nayo, futa, tupa ►Soma zaidi
Kichwa chake ni kidogo zaidi ukilinganisha na wanyama wengine wa jamii yake kama chui. Duma anatofautiana na chui pia kwa sehemu ya mgongo na sehemu ya machoni: mgongo wa duma huwa kama alama ya "S", tofauti na mgongo wa chui. Macho ya duma yana weusi mkali ukilinganisha na chui.
Ngozi yake ina rangi ya manjano inayoelekea kwenye rangi ya udongo iliyopambwa na madoa meusi. Rangi ya duma inashabihiana na mazingira yake ya mawindo hutegemea zaidi mbio na kuona ukilinganisha na wanyama wengine wawindaji ambao hutegemea kunusa na kuvizia katika mawindo yao. Ndiye mnyama anayeaminika kuwa na mwendo kasi zaidi kuliko wanyama wengine watembeao kwa miguu: hukimbia kilometa 113 kwa saa.
Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili
Idadi ya makala: 74,866
Idadi ya kurasa zote: 151,588 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
Katika mwezi wa Agosti 2020 wikipedia ya Kiswahili iliangaliwa mara milioni 1.73 hivi, ambayo ni sawa na mara 55,800 kwa siku au mara 2,326 kila saa. Asilimia 52 za wasomaji wetu wako Tanzania, asilimia 13 wako Kenya, asilimia 18 wako Marekani na mnamo asilimia 10 wako Ulaya.
(fungua anwani kwa browser yako, ondoa majina yaliyopo na ingiza jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa)
na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani.
(unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)
Kamusi elezo ya Wiki ni kamusi elezo huru iliyo chini ya Shirika Lisilo la Kiserikali la Wikimedia Foundation, ambalo linasimamia miradi mingine mbalimbali ambayo imeorodheshwa hapo chini. Mpaka sasa miradi inayopatikana Kiswahili ni Wikipedia na Wikamusi. Wikitabu imewekwa Kiswahili lakini bado ni tupu. Mengine inapatikana Kiingereza pamoja na lugha tofauti.
↑About prevention and treatment, tovuti ya National Center for Immunization and Respiratory Diseases (NCIRD), Division of Viral Diseases, Marekani, iliangaliwa 30 Januari 2020