Chakula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Vyakula vyenye asili ya mimea.
Aina za nyama.

Chakula (kifupi cha "kitu cha kula", kutoka kitenzi "kula") ni kile kinacholiwa na watu kwa kudumisha na kustawisha uhai wao. Ni kwamba mwili unahitaji virutubishi, nishati na maji. Hayo yote hupatikana katika chakula.

Virutubishi vya mwili ni hasa yafuatayo:

Protini, mafuta na wanga huleta nishati ya mwili. Vilevile hukuza mwili yaani katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula (tumboni) vinapasuliwa kwa sehemu asilia zake na kuingizwa katika muundo wa seli za mwili.

Chakula kinaweza kutoka kwenye mimea au kwenye wanyama. Sehemu ya mahitaji yanatoka pia moja kwa moja kwenye mazingira bila kupitia mimea wala wanyama, hasa madini, kwa mfano chumvi.

Lakini chakula si kazi ya kibiolojia na kifiziolojia pekee, bali kina upande wa kiutamaduni na kijamii vilevile.

Kila nchi ina chakula chake na watu wamezoea vyakula pamoja na namna ya kutayarisha vyakula vyao.

Chakula na afya

Chakula kinatakiwa kuwa na sehemu zote zinazohitajiwa na mwili. Uhaba wa sehemu moja utasababisha utapiamlo na magonjwa mbalimbali. Kuna matatizo hasa kama watoto hukosa chakula chenye ulinganifu. Mara nyingi wakinamama wanaowapa watoto chakula wanajali tu ya kwamba mtoto ashibe. Mtu anaweza kushiba kutokana na wanga peke yake lakini uhaba wa protini na vitamini huleta utapiamlo na kusababisha magonjwa na ikitokea kwa watoto upungufu wa kukua kwa sehemu za ubongo na mwili.

Vilevile kuna tatizo la mara kwa mara: ni uhaba wa minerali fulani katika mazingira ya pekee.

Chakula kinahusiana na afya pia kuhusu wingi au uhaba wake. Inaeleweka ya kwamba uhaba wa chakula yaani njaa ya muda mrefu inadhoofisha mwili na afya. Lakini kinyume chake kuzidi kwa chakula kunaleta hatari pia. Katika maisha ya mjini na familia waliotoka katika umaskini kali hali ya kunenepa tangu utotoni imekuwa tatizo kubwa. Kunenepa mno kunafupisha maisha na kuandaa mwili kwa magonjwa mengi yasiyotokea kwa uzito wa wastani mwilini.

Vyanzo

Vyakula vingi hutokana na mimea. Hata wanyama ambao hutumiwa kama chakula kwa binadamu huwa wanafugwa na kupewa vyakula vinavyotokana na mimea. Hivi sasa asilimia 75 ya vyakula vinavyoliwa na binadamu vinatokana na wanyama 5 na mimea 12 tu. [1]

Walaji mboga hukataa chakula chochote chenye nyama au mafuta ya kinyama kwa sababu za kidini au kimaadili.

Mahindi, ngano, na mchele ndio asilimia 87 ya nafaka inayotumiwa kwa chakula duniani.[2][3][4] Hata hivyo asilimia kubwa ya nafaka inayopandwa duniani hutumika kwa malisho ya wanyama.

Ngano ndiyo nafaka yenye nishati ya juu kuliko vyakula vyote duniani.[5]

Vyakula vya binadamu
Asili ya mimea Asili ya wanyama

Marejeo

Viungo vya nje

Wikiquote-logo.svg
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:

Wikivoyage-Logo-v3-icon.svg Chakula travel guide kutoka Wikisafiri

Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chakula kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.