Ni vipi ninaweza kurekebisha jinsi ninaonyeshwa matangazo kwenye Facebook kutegemea data kuhusu shughuli yangu kutoka kwa washirika?

Ili kukuonyesha matangazo muhimu, tunapokea na kutumia data ambayo watangazaji na washirika wengine wanatupatia kuhusu shughuli yako kwenye tovuti na programu zao, na pia baadhi ya miingiliano yako ya nje ya mtandao, kama vile ununuzi. Kwa mfano, tunaweza kukuonyesha tangazo la shati kulingana na ziara yako kwenye tovuti ya nguo.
Unaweza kudhibiti ikiwa unaona matangazo kulingana na shughuli zako nje ya Facebook, kupitia Data Kuhusu Shughuli Yako Kutoka kwa Washirika katika Mapendeleo yako ya Matangazo.
Kutazama na kurekebisha mpangilio huu:
  1. Donoa account kwenye upande wa juu kulia wa Facebook.
  2. Teua Mpangilio na Faragha, kisha ubofye Mipangilio.
  3. Telezesha chini na ubofye Matangazo katika menyu iliyo kushoto.
  4. Bofya Mipangilio ya Matangazo, kisha bofya Data kuhusu shughuli kutoka kwa washirika wako.
  5. Teua ikiwa tunaweza kutumia data kutoka kwa washirika wetu kukuonyesha matangazo.
Kumbuka, mpangilio huu hudhibiti kama tunaweza kukuonyesha matangazo yaliyogeuzwa kukufaa kwenye Facebook kutegemea data kuhusu shughuli yako kwenye Facebook. Ukizima mpangilio huu, huenda matangazo unaona bado yanategemea shughuli yako kwenye jukwaa letu. Huenda pia yanategemea maelezo kutoka kwa biashara maalum ambayo imeshiriki orodha ya watu au vifaa nasi, ikiwa tumelinganisha wasifu wako na maelezo kwenye orodha hiyo.
Mpangilio huu unatekelezwa tu kwa matangazo unayoyaona kwenye akaunti yako ya Facebook, ikijumuisha kwenye Messenger, na kwa matangazo unayoyaona kwenye tovuti, programu na vifaa vinavyowasilishwa na huduma za utangazaji za Facebook. Mpangilio huu hautekelezwi kwa matangazo unayoyaona kwenye Instagram, isipokuwa uwezeshe tajiriba iliyounganishwa kwenye akaunti zako za Instagram na Facebook. Jifunze jinsi ya kurekebisha jinsi ambavyo unaonyeshwa matangazo kwenye Instagram.
Iwapo umewezesha tajiriba iliyounganishwa kwenye akaunti zako za Instagram na Facebook, unaweza pia kurekebisha tajriba yako ya tangazo la Facebook kupitia mpangilio wa Data Kuhusu Shughuli Yako Kutoka kwa Washirika.
Tunazingatia Kanuni za Kujidhibiti kwa Utangazaji wa Mwenendo wa Mtandaoni na kushiriki katika programu za kuchagua kuondoka zilizozinduliwa na Digital Advertising Alliance, Digital Advertising Alliance of Canada na European Interactive Digital Advertising Alliance. Unaweza kuchagua kuondoka kwenye kampuni zote zinazoshiriki kupitia tovuti hizi.
Je, hii ilikusaidia?
Ndiyo
La