Wikipedia:Ukurasa wangu na kurasa za kamusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ukurasa wa mtumiaji ni ukurasa wako. Hapo uko huru kuandika juu yako mwenye unachotaka.

Kanuni ni tofauti katika kurasa za kawaida yaani kurasa za kamusi (ing.: Article space). Hapa ni marufuku kuandika juu yako mwenyewe. Kuna ruhusa moja tu: kama wewe uliandika kitabu au kutoa wimbo unaweza kuingiza habari hii kama marejeo katika makala iliyopo tayari. Lakini usianzishe wewe mwenyewe!

Maana hapa tuko kwenye kamusi elezo, si Facebook au mtandao wa kijamii. Sisi wachangiaji tunawasiliana kati yetu kwa kutumia kurasa za majadiliano na ukurasa wa jamii, pia kwa barua pepe.

Afadhali ulizia maswali yako kwanza kwa Wakabidhi, tuko tayari kukusaidia!

Kuhariri ukurasa wako

Nenda kwa "Mapendekezo" hapo juu kwenye ukurasa wako.

Ukibofya hapo unaweza kuamulia tabia mbalimbali jinsi unavyoonekana na kupatikana kwa watumiaji wengine wa wikipedia.

Unaweza kuchagua

  • Maelezo ya kimsingi (pamoja na kubadilisha neno la siri)
  • Lugha
  • Hitiari za barua pepe (kama wengine wanaruhusiwa kukuandikia email kupitia wikipedia au la)

Tahadhari kuhusu ukurasa wako

Tahadhari moja kuhusu ukurasa wako: tafakari vema unachotaka kutangaza juu yako! Tafakari kama ni vema kutaja jina lako halisi. Ukifanya kazi na kuwa na mwajiri - labda itakusaidia au kuleta hasara kama bosi wako anajua unatumia muda wako kwenye wikipedia (hasa kama unahariri kutoka ofisini! - wengine hawapendi). Basi utaamua mwenyewe!