Mwanzo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Karibu kwenye Wikipedia,
Hadi leo tuna makala takriban 58,969 kwa Kiswahili
     

     

Kamusi Elezo ya Kiswahili

Karibu kwenye Wikipedia ya Kiswahili!

Wikipedia ni mradi wa kuandika kamusi elezo kamili na sahihi ya maandishi huru.

Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na kufungua akaunti. Angalia Wikipedia:Mwongozo ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.


Je, wajua...

Kutoka kwenye mkusanyiko wa makala za Wikipedia:

Ngorongoro

  • ... kwamba Kimondo cha Mbozi ni jiwe kubwa kutoka anga la nje linaloweza kuangaliwa huko Mbozi?
  • ... kwamba Asha-Rose Mtengeti Migiro alikuwa mwanasiasa wa kwanza kutoka nchini Tanzania kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa?
  • ... kwamba Calestous Juma aliaga dunia akiwa profesa wa kwanza kutoka nchini Kenya kwenye Chuo Kikuu cha Harvard, Marekani?


  • Makala ya wiki

    Kassim Mapili

    Kassim Said Mapili (1937 - 2016) alikuwa mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi kutoka nchini Tanzania. Mzee Mapili alizaliwa katika kijiji cha Lipuyu, Tarafa ya Lionya, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi mwaka 1937. Hivyo umauti umekuta Mzee Mapili akiwa na umri wa miaka 79. Alipata elimu ya msingi huko kwao Lipuyu, sambamba na kupata elimu ya dini na mwenyewe aliwahi kusema alianza kupata mapenzi ya kuimba wakati alipokuwa Madrasa akighani Kaswida. Mwaka 1958 alijiunga na White Jazz Band iliyokuwa na masikani yake huko Lindi.

    Mwaka mmoja baadaye akahamia Mtwara na kujiunga na Mtwara Jazz Band, lakini mwaka 1962 akajiunga na Honolulu Jazz Band ambayo nayo ilikuwa hapo hapo Mtwara. Mwaka 1963, Mzee Mapili akachukuliwa na TANU Youth League ya mjini Lindi, na kujiunga na bendi ya Jamhuri Jazz Band ya hapo Lindi. Mwaka 1964 Mzee Mapili akachaguliwa kuanzisha bendi ya TANU Youth League ya Tunduru. Mwaka mmoja baadaye alihamia Kilwa Masoko na kujiunga na Lucky Star Jazz Band ya mji huo. ►Soma zaidi


    Picha nzuri ya wiki

    Duma

    Duma ni mnyama mbuai aliyemo katika jamii ya paka (Felinae). Chakula chake ni wanyama jamii ya swala hupatikana Afrika na kidogo sehemu za Asia.

    Kichwa chake ni kidogo zaidi ukilinganisha na wanyama wengine wa jamii yake kama chui. Duma anatofautiana na chui pia kwa sehemu ya mgongo na sehemu ya machoni: mgongo wa duma huwa kama alama ya "S", tofauti na mgongo wa chui. Macho ya duma yana weusi mkali ukilinganisha na chui.

    Ngozi yake ina rangi ya manjano inayoelekea kwenye rangi ya udongo iliyopambwa na madoa meusi. Rangi ya duma inashabihiana na mazingira yake ya mawindo hutegemea zaidi mbio na kuona ukilinganisha na wanyama wengine wawindaji ambao hutegemea kunusa na kuvizia katika mawindo yao. Ndiye mnyama anayeaminika kuwa na mwendo kasi zaidi kuliko wanyama wengine watembeao kwa miguu: hukimbia kilometa 113 kwa saa.

    Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili

    • Idadi ya makala: 58,969
    • Idadi ya kurasa zote: 120,463 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
    • Idadi ya hariri: 1,110,365
    • Idadi ya watumiaji waliojiandikisha: 42,243
    • Idadi ya wakabidhi: 11
    • Idadi ya watumiaji hai: 131 (Watumiaji waliojiandikisha na kuchangia katika muda wa siku 30 zilizopita)

    Bofya hapa kwa kupata namba za sasa
    Angalia idadi ya wasomaji kwa makala mbalimbali
    (fungua anwani kwa browser yako, badilisha "Mwanzo" kwa jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa)
    • na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani.
    (unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)

    Michango ya wanawiki: angalia hapa michango ya mtumiaji kwenye kila mradi wa Wikimedia (andika jina la mtumiaji kwenye sanduku)

    Jumuia za Wikimedia

    Commons
    Ghala ya Nyaraka za Picha na Sauti
    Meta-Wiki
    Uratibu wa Miradi yote ya Wikimedia
    Wiktionary-logo.svg
    Wikamusi
    Kamusi na Tesauri
    Wikibooks-logo.png
    Wikitabu
    Vitabu vya bure na Miongozo ya Kufundishia
    Wikiquote-logo-51px.png
    Wikidondoo
    Mkusanyiko wa Nukuu Huria
    Wikisource-logo.png
    Wikichanzo (Wikisource)
    Matini za vyanzo asilia kwa Kiswahili
    Wikispishi
    Kamusi ya Spishi
    Graduation cap.png
    Wikichuo
    Jumuia ya elimu
    Wikinews-logo.png
    Wikihabari
    Habari Huru na Bure