Austria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
'Republik Österreich
Jamhuri ya Austria
Bendera ya Austria Nembo ya Austria
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: “'Land der Berge, Land am Strome
(Kijerumani kwa "Nchi ya milima, nchi ya mtoni")
Lokeshen ya Austria
Mji mkuu Vienna
48°12′ N 16°21′ E
Mji mkubwa nchini Vienna
Lugha rasmi Kijerumani 1
Serikali Jamhuri
Alexander Van der Bellen
Sebastian Kurz
Uhuru
Mkataba kuhusu Austria ulianza
Tangazo la baki

27 Julai 1955
26 Oktoba 1955
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
83,871 km² (ya 115)
1.3
Idadi ya watu
 - 2006 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
8,292,322 (ya 9)
8,032,926
99/km² (ya 99)
Fedha Euro () 2 (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .at 3
Kodi ya simu +43
1 Kislovenia, Kikroatia, Kihungaria ni lugha rasmi kieneo.
2 Kabla ya 1999: Shilingi ya Austria.



Ramani ya Austria

Austria (kwa Kijerumani: Österreich) ni nchi ya Ulaya ya Kati. Imepakana na Ujerumani, Ucheki, Slovakia, Hungaria, Slovenia, Italia, Uswisi na Liechtenstein.

Mji mkuu ni Vienna.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Austria:Uso wa nchi
Mlima Grossglockner

Eneo la nchi lina umbo ndefu na nyembamba kama kanda linaloelekea kutoka mashariki kwenda magharibi.

Sehemu kubwa ya Austria (60%) ni milima. Tambarare ziko hasa kando la mto Danubi ambao ni pia mto mkubwa. Theluthi moja ya eneo liko chini ya mita 500 juu ya usawa wa bahari. Zaidi ya 40% za nchi ni misitu. Mto Danubi unavuka sehemu kubwa ya nchi.

Milima mikubwa ya Austria inafikia kimo kati ya mita 3000 na 4000. Katika hali ya hewa ya nchi kuna theluji mwaka wote. Mlima mkubwa ni Grossglockner wenye mita 3,798, halafu Wildspitze wenye mita 3,774 juu ya UB.

Ziwa kubwa ni ziwa la Neusiedler See lililopo mpakani kwa Hungaria. Mlimani kuna maziwa mengi madogo.

Uso huo wa nchi ni msingi wa utalii ulio muhimu sana Austria. Wakati wa joto watalii wanaponda baridi ya milima; wakati wa baridi wanakuja kucheza ski.


Majimbo[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: Majimbo ya Austria
Nafasi Jimbo Makao
makuu
Jina rasmi Wakazi Eneo (km²)
1 Vienna Vienna Wien 1,677,867 415
2 Austria Chini Sankt Pölten Niederösterreich 1,597,240 19,178
3 Austria Juu Linz Oberösterreich 1,408,165 11,982
4 Steiermark Graz Steiermark 1,205,609 16,392
5 Tirol Innsbruck Tirol 703,512 12,648
6 Karinthia Klagenfurt Kärnten 561,094 9,536
7 Salzburg Salzburg Salzburg 530,576 7,154
8 Vorarlberg Bregenz Vorarlberg 366,377 2,601
9 Burgenland Eisenstadt Burgenland 281,190 3,965

Miji[hariri | hariri chanzo]

Hali halisi kuna jiji moja tu ambalo ni mji mkuu Wien (Vienna). Ulikua kama mji mkuu wa Kaisari wa Dola Takatifu la Kiroma na baadaye wa milki ya Austria iliyojumlisha sehemu kubwa za Ulaya ya Kusini-Mashariki.

Miji mingine mikubwa kiasi ni

Historia[hariri | hariri chanzo]

Austria kama nchi ndogo jinsi ilivyo sasa imepatikana mwaka 1918 na tena tangu 1945.

Kwa muda mrefu wa historia yake Austria ilihesabiwa kama sehemu ya Ujerumani. Kwa karne nyingi watawala wake walishika cheo cha Kaisari wa Dola takatifu la Roma lililojumlisha Ujerumani wote.

Austria ilitawala pia sehemu kubwa za Ulaya ya Mashariki. Watawala wa Austria walishika pia vyeo vya kifalme vya nchi za Bohemia na Hungaria.

Wakati wa vita za Napoleoni Kaisari Franz II alilazimishwa kujiuzulu kama Kaisari wa Ujerumani wote mwaka 1806 akabaki na cheo cha Kaisari wa Austria tu. Baada ya Napoleoni Austria ilikuwa nchi muhimu katika shirikisho la Ujerumani.

Mwaka 1866 Austria ilishindwa katika vita dhidi ya Prussia ikatoka katika siasa ya Ujerumani. Baada ya vita hiyo Kaisari Franz-Josef alipaswa kuwakubalia Wahungaria cheo sawa na Wajerumani ndani ya milki yake. Kuanzia hapo milki ilijulikana kama Austria-Hungaria

Hadi Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia Austria-Hungaria iliendelea kutawala nchi za Ulaya ya Mashariki pamoja na Ucheki, Slovakia, Slovenia, Kroatia, Bosnia-Herzegovina, na sehemu kubwa ya Poland ya Kusini, pia sehemu zilizopo sasa katika kaskazini mwa Italia.

Mwisho wa vita dola hili lilisambaratishwa. Sehemu zake zote zikawa nchi huru. Nchi ndogo ambayo ilikaliwa na Waaustria Wajerumani ilibaki. Washindi wa vita walizuia Waaustria wasijiunge na Ujerumani, hivyo Jamhuri ya Austria ilianzishwa.

Mwaka 1938 dikteta wa Ujerumani Adolf Hitler (aliyekuwa Mwaustria mwenyewe) alivamia Austria kwa jeshi lake na kuiunganisha na Ujerumani. Wakati ule sehemu kubwa ya Waaustria walikubali.

Baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia Austria ilirudishwa kuwa nchi ya pekee ikabaki hivyo.

Mwaka 1995 Austria ikajiunga na Umoja wa Ulaya.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Watu wa Austria huzungumza Kijerumani ambacho ni pia lugha rasmi. Mpakani upande wa kusini na mashariki kuna pia wasemaji wa Kikroatia, Kislovenia na Kihungaria. Lugha hizi zina cheo rasmi kieneo au kitarafa.

Kwa jumla lahaja na utamaduni hufanana katika mengi na ile ya Wabavaria katika jimbo la jirani la Ujerumani. Kama huko wananchi wengi ni Wakatoliki (77%) na Wakristo wengine (9%).

Waaustria mashuhuri duniani[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufalme wa Muungano | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Austria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.