Vidokezo vya kutiririsha

Makala haya hutoa ushauri muhimu kuhusu kuweka mipanglio ya mtandao wako, kutumia kamera ya wavuti na kuandaa programu yako ya kusimba ili upate mtiririko mubashara ulio bora kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuanza kutiririsha mubashara.

Intro To Live Streaming on YouTube

Kuweka mipangilio ya mtandao

  • Kuwa na kipimo data cha kutosha: Jumla ya kasi ya biti unayotiririsha haiwezi kuzidi kiasi cha kipimo data cha upakiaji kinachopatikana. Acha nafasi kiasi (tunapendekeza asilimia 20).
  • Kuwa na muunganisho wa kasi ya juu: Huenda ofisi yako ikawa na muunganisho wa kasi ya juu, lakini ikiwa watu wengi wanatumia mtandao huo, muunganisho wako unaweza kuwa hafifu.
  • Fanya jaribio la kasi: Kipimo cha data cha kupakua (kasi ya upakuaji) mara nyingi ni kikubwa kuliko cha kupakia (kasi ya kupakia). Hakikisha kuwa muunganisho wako unapopakia unatosha kutuma kasi yako ya biti ya kutiririsha. Tunapendekeza msingi + akiba + asilimia 20.
  • Kuwa na mtandao unaoaminika: Kukatika kwa muunganisho wako kutamaanisha mtiririko wako utakatika.

Kutumia kamera ya wavuti

  • Ubora wa mtiririko: Unaweza kutiririsha ukitumia kompyuta ya kupakata na kamera ya wavuti, lakini ukitumia vifaa bora, utapata mtiririko mubashara ulio bora.
  • Programu ya kusimba: Unaweza kutumia programu ya usimbaji kama vile Wirecast au Kamera ya wavuti ya YouTube.
  • Kiwango cha utayarishaji: Kwa matukio ya utayarishaji yaliyo na idadi kubwa ya mitiririko, tunapendekeza utumie programu za maunzi za kusimba zilizo na kiwango cha kitaalamu.
  • Fanyia mipangilio yako jaribio: Hakikisha kuwa umeifanyia mipangilio yako jaribio la kutosha kabla ya tukio.

Kutumia usimbaji

  • Weka mtiririko mapema: Weka mipangilio ya programu ya kusimba katika mtiririkomubashara angalau saa 2 kabla ya mtiririko kuanza.
  • Weka programu ya kusimba mapema: Anzisha programu za kusimba angalau dakika 15 kabla ya tukio kuratibiwa kuanza.
  • Kagua mtiririko wako: Kabla ya kubofya Anza Kutiririsha, angalia onyesho la kukagua kwenye Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja.
  • Weka programu mbadala ya kusimba: Kwa jaribio la programu ya kusimba ambalo halikufanikiwa, simamisha programu kuu ya kusimba (au uchomoe kebo yake ya Ethaneti) na uhakikishe kuwa kichezaji kinafikia programu mbadala ya kusimba.
  • Angalia faili za kumbukumbu zilizopo: Thibitisha uadilifu wa faili zote za kumbukumbu zilizo kwenye kifaa. Hakikisha kuwa ukubwa wa faili ya kumbukumbu iliyopo kwenye kifaa unaongezeka.
  • Angalia iwapo mtiririko mubashara unaonekana: Thibitisha kuwa tukio linaweza kufikiwa kupitia chaneli na kurasa za kutazama.
  • Angalia mtiririko mubashara kwenye simu: Thibitisha kuwa tukio linaweza kufikiwa kupitia vifaa vya mkononi.
  • Angalia sauti na video: Fuatilia mitiririko kila mara ili uone ubora wa sauti na video.
  • Baada ya kumaliza, simamisha programu ya kusimba: Baada ya tukio kukamilika kwenye YouTube, simamisha programu ya kusimba.

Kudumisha usalama katika mitiririko mubashara

  • Maudhui: Fahamu aina za video za kutiririsha. Unaporekodi video za marafiki, watu mnaosoma nao au vijana, kumbuka kwamba video hizo hazipaswi kuwa za kuchochea ngono, za vurugu au hatari.
    • Kumbuka kuwa kanuni hii pia inatumika kwenye gumzo la moja kwa moja. Pata maelezo zaidi kuhusu Mwongozo wetu wa Jumuiya.
  • Taarifa binafsi: Kuwa makini kuhusu kutuma taarifa yoyote binafsi unapotiririsha mubashara na katika Gumzo la Moja kwa Moja. Ufikiaji wa msimamizi wa chaneli yako unapaswa kupewa tu kwa wale unaowaamini. YouTube haitakuomba idhini za udhibiti katika mtiririko wako.
  • Udhibiti: Ripoti video zisizofaa au uzuie watumiaji wanaokufanya wewe au wengine kutohisi vyema kushiriki kwenye gumzo. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti gumzo la moja kwa moja.
  • Faragha: YouTube ina vipengele vya kukusaidia kudhibiti wanaoweza kuona mitiririko mubashara unayochapisha. Linda faragha yako kwa kuweka mitiririko mubashara ya kibinafsi iwe "ya faragha" au "haijaorodheshwa." Tumia ukurasa wa Mipangilio ya faragha na usalama ili uone zana zinazoweza kukusaidia kudhibiti utumiaji wako kwenye tovuti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
8771529624115384337
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false