Beji za uthibitishaji kwenye vituo

Unapoona au alama ya kuteua ya kuthibitisha kando ya jina la kituo cha YouTube, inamaanisha kuwa YouTube imethibitisha kituo hicho.

Kutuma maombi ya uthibitishaji wa chaneli

You can submit a request for a channel verification once you have 100,000 subscribers. It looks like your channel isn't eligible yet.

Make sure you're signed in with the email address for the eligible channel. Click your profile picture in the top-right and choose that account.

To see if your channel is eligible to request verification, click Sign in at the top-right. 

Hatutathibitisha vituo ambavyo vinajaribu kuiga mtayarishi au chapa nyingine. Tukikuta kituo kinachojaribu kuiga mtu mwingine kwa makusudi, huenda tukachukua hatua zaidi.

Kuhusu vituo vilivyothibitishwa

Iwapo kituo kimethibitishwa, ni kituo rasmi cha mtayarishi, msanii, kampuni au mtu maarufu. Chaneli zilizothibitishwa husaidia kutofautisha chaneli rasmi kutoka chaneli zingine zenye majina yanayofanana kwenye YouTube.

Kumbuka:

  • Vituo vilivyothibitishwa havipati vipengele vya ziada kwenye YouTube. Pia, haviwakilishi tuzo, malengo au kuidhinishwa kutoka YouTube. Kwa maelezo kuhusu tuzo, pata maelezo zaidi kuhusu mpango wa Tuzo za Watayarishi wa YouTube.
  • Ikiwa kituo chako kimethibitishwa, kitaendelea kuonyesha hali ya kuthibitishwa usipobadilisha jina la kituo chako. Ukibadilisha jina la kituo chako, kituo ulichobadilisha jina hakitathibitishwa, utahitaji kutuma maombi upya.
  • Kubadilisha kitambulishi cha kituo chako hakutaondoa beji yako ya uthibitishaji.
  • YouTube inahifadhi haki ya kubatilisha uthibitishaji au kufunga vituo vinavyokiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya au Sheria na Masharti ya YouTube.
  • Uthibitishaji umebadilika katika kipindi cha muda, hivyo huenda ukaona aina nyingi za vituo zikiwa na uthibitishaji kwenye YouTube.

Ustahiki wa kituo kilichothibitishwa

Ili ustahiki kutuma maombi ya kuthibitishwa, ni sharti kituo chako kifikishe watu 100,000 wanaofuatilia.

Baada ya kutuma maombi, tutakagua kituo chako. Tunathibitisha vituo ambavyo:

  • Ni halisi: Ni sharti kituo chako kiwakilishe mtayarishaji, chapa au huluki halisi ambaye kinatambulisha. Tutakagua vigezo tofauti ili kusaidia kuthibitisha utambulisho wako, kama vile umri wa kituo chako. Huenda pia tukaomba hati au maelezo zaidi.
  • Zimekamilika: Ni sharti chaneli yako iwe ya umma na iwe na bango la chaneli, maelezo na picha ya wasifu. Kituo kinahitaji pia kuwa na maudhui na kiwe kinachapisha na kushirikisha hadhira yake mara kwa mara kwenye YouTube.

Wakati mwingine, huenda YouTube pia ikathibitisha kwa hiari yake vituo vilivyo na chini ya watu 100,000 wanaofuatilia ambavyo vinajulikana vizuri nje ya YouTube.

Tofautisha akaunti yako bila uthibitishaji

Ikiwa kituo chako hakijathibitishwa, hizi ni baadhi ya njia nyingine za kutofautisha kituo chako kutoka vituo vinavyofanana:

Ikiwa mtu anakuiga wewe au kituo chako, mripoti kwetu.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu
1844015383370026631
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false