Takwimu

Utazamaji

  • Zaidi ya watumiaji mahususi bilioni 1 hutembelea YouTube kila mwezi
  • Zaidi ya saa bilioni 6 za video hutazamwa kila mwezi kwenye YouTube-hiyo ni karibu saa moja kwa kila mtu duniani
  • Saa 100 za video hupakiwa kwenye YouTube kila dakika
  • Asilimia 80 ya utazamaji wa YouTube hutoka nje ya Marekani
  • YouTube imejanibishwa katika nchi 61 na lugha 61
  • Kulingana na Nielsen, YouTube huwafikia watu wazima wengi Marekani wa umri wa miaka 18-34 kuliko mtandao mwingine wowote wa kebo
  • Mamilioni ya usajili hufanyika kila siku. Idadi ya watu wanaojisajili kila siku imeongezeka kwa zaidi ya mara 3 tangu mwaka jana, na idadi ya wanaojisajili kila siku kufuatilia imeongezeka kwa zaidi ya mara 4 tangu mwaka jana

Mpango wa Washirika wa YouTube

  • Iliundwa mwaka wa 2007, sasa tuna zaidi ya waundaji milioni moja kutoka zaidi ya nchi 30 kote ulimwenguni wanaopata pesa kutokana na video zao za YouTube
  • Maelfu ya vituo hugonga takwimu sita kila mwaka

Uchumaji wa mapato

  • Maelfu ya watangazaji wanatumia mtiririko wa TrueView na asilimia 75% ya matangazo yetu ya ndani ya mtiririko sasa yanaweza kurukwa
  • Tuna watangazaji zaidi ya milioni wanaotumia mifumo ya uendeshaji ya Google ad, wengi ambao ni wafanyabiashara ndogondogo

Simu ya mkononi na Vifaa

  • Vifaa vya mkononi huchangia hadi asilimia 40 ya muda wa kutazama YouTube kote duniani
  • YouTube inapatikana katika mamia ya mamilioni ya vifaa

Content ID

  • Content ID huchanganua zaidi ya miaka 400 ya video kila siku
  • Zaidi ya washirika 5,000 hutumia Content ID, ikiwa ni pamoja na mitandao mikuu ya utangazaji Marekani, studio za filamu na kampuni za mziki
  • Tuna zaidi ya faili milioni 25 za marejeleo katika hifadhidata yetu ya Content ID; ni miongoni mwa faili pana zaidi duniani
  • ContentID imezalisha mamia ya mamilioni ya dola kwa washirika