Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na kufungua akaunti. Angalia Wikipedia:Mwongozo ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.
Hamed bin Mohammed el Murjebi (1837 – 14 Juni1905) amejulikana zaidi kwa jina la Tippu Tip. Alikuwa mfanyabiashara mashuhuri katika Afrika ya Mashariki na Kati wakati wa karne ya 19.
Babake alikuwa mfanyabiashara Mwarabu Muhammed bin Juma, mamake aliitwa Nyaso. Hamed aliingia katika shughuli za biashara tangu umri wa miaka 12 akafaulu katika biashara ya misafara kati ya Zanzibar na Kongo. Alipanga misafara ya mahamali waelfu akipeleka bidhaa kutoka Bagamoyo kupitia Tabora hadi Ujiji kwa Ziwa Tanganyika na ndani ya Kongo. Bidhaa alizobeba alitumia kujipatia pembe za ndovu na watumwa; watumwa walisaidia kubeba pembe za ndovu njia ya kurudi hadi pwani. Hemed alitajirika sana. Athira yake ilipanuka katika Kongo ya Mashariki hadi alitawala eneo kubwa sana.
Ng'ombe ni wanyama wakubwa wa jenasi Bos. Spishi ya ng'ombe ina nususpishi au aina nyingi lakini ni spishi moja tu.
Ng'ombe hula manyasi na kutembea kwa vidole viwili.
Asili yake ni aina za ng'ombe wa pori waliofugwa kwa sababu ya nyama na maziwa. Katika nchi nyingi anatumiwa pia kama mnyama wa mizigo anayevuta plau au magari.
Wataalamu huamini ya kwamba aina zote za ng'ombe zina asili katika mashariki ya kati mnamo milenia ya 9 KK ambako watu waliwahi kuwafuga nas kutoka hapa ufugaji ng'ombe ulisambaa kote duniani.
Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili
Idadi ya makala: 51,335
Idadi ya kurasa zote: 108,212 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
(fungua anwani kwa browser yako, badilisha "Mwanzo" kwa jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa)
na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani.
(unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)
Jumuia za Wikimedia
Kamusi elezo ya Wiki ni kamusi elezo huru iliyo chini ya Shirika Lisilo la Kiserikali la Wikimedia Foundation, ambalo linasimamia miradi mingine mbalimbali ambayo imeorodheshwa hapo chini. Mpaka sasa miradi inayopatikana Kiswahili ni Wikipedia na Wikamusi. Wikitabu imewekwa Kiswahili lakini bado ni tupu. Mengine inapatikana Kiingereza pamoja na lugha tofauti.