Wakati askari hao wakijaribu kumnasihi Mnyika kutoka nje ya ukumbi wa Bunge kwa hiari yake, spika Job Ndugai alisema: “Nyinyi askari gani toa nje, askari wa wapi hawa, nyinyi ni askari au raia, ukiambiwa toa mtu toa mtu…,” alisema kwa hasira. Baada ya karipio hilo la spika askari hao waliongeza kasi na kumburuza Mnyika hadi nje huku Mbunge wa Kawe Halima Mdee akijaribu