Mwanzo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Karibu kwenye Wikipedia,
Hadi leo tuna makala takriban 35,790 kwa Kiswahili
     

     

Kamusi Elezo ya Kiswahili

Karibu kwenye Wikipedia ya Kiswahili!

Wikipedia ni mradi wa kuandika kamusi elezo kamili na sahihi ya maandishi huru.

Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na kufungua akaunti. Angalia Msaada wa kuanzisha makala ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.


Je, wajua...

Kutoka kwenye mkusanyiko wa makala za Wikipedia:

Ngorongoro



Makala ya wiki

(maelezo ya picha)

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) (ing. Tanzania People's Defense Force TPDF) ni jeshi lililoanzishwa mnamo mwezi wa Septemba katika mwaka wa 1964. Ilichukua nafasi ya jeshi la Tanganyika Rifles lililorithiwa na ukoloni wa Kiingereza. Chanzo cha jeshi nchini Tanzania kilikuwa jeshi la kikoloni la Uingereza katika Afrika ya Mashariki. Mwaka 1919 Uingereza ilikabidhiwa utawala juu ya Tanganyika na Shirikisho la Mataifa. Baada ya uhuru mwaka 1961 vikosi vya King's African Rifles katika Tanganyika vilibadilishwa jina na kuwa Tangayika Rifles (TR). Pamoja na kubadilika jina Tanganyika Rifles ilikuwa na muundo sawa na Kings African Rifles (KAR). Maafisa wenye mamlaka bado walikuwa Waingereza, pamoja na Waafrika watano waliopandishwa cheo wakati wa uhuru na kupokea mafunzo katika vyuo vya kijeshi vya Kiingereza. Jeshi jipya lilipangwa katika vikosi viwili vyenye makao makuu huko Dar es Salaam na Tabora. Afisa mkuu alikuwa Brigedia Jenerali Patrick Sholto Douglas. Kwa jumla kulikuwa na hali ya kutoridhika kati ya askari wa TR. Sababu yake ilikuwa matumaini ya kwamba uhuru ungeleta mabadiliko makubwa zaidi na nafasi za kupanda cheo baada ya kuondoka kwa maafisa wazungu. Lakini maafisa Waingereza waliendelea kuajiriwa na serikali ya Nyerere na tofauti kubwa katika mapato na hali ya makazi ya Wazungu na Waafrika ziliendelea. ►Soma zaidi


Picha nzuri ya wiki

Ng'ombe

Ng'ombe ni wanyama wakubwa wa jenasi Bos. Spishi ya ng'ombe ina nususpishi au aina nyingi lakini ni spishi moja tu.

Ng'ombe hula manyasi na kutembea kwa vidole viwili. Asili yake ni aina za ng'ombe wa pori waliofugwa kwa sababu ya nyama na maziwa. Katika nchi nyingi anatumiwa pia kama mnyama wa mizigo anayevuta plau au magari.

Wataalamu huamini ya kwamba aina zote za ng'ombe zina asili katika mashariki ya kati mnamo milenia ya 9 KK ambako watu waliwahi kuwafuga nas kutoka hapa ufugaji ng'ombe ulisambaa kote duniani.

Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili

  • Idadi ya makala: 35,790
  • Idadi ya kurasa zote: 85,052 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
  • Idadi ya hariri: 1,037,136
  • Idadi ya watumiaji waliojiandikisha: 26,596
  • Idadi ya wakabidhi: 9
  • Idadi ya watumiaji hai: 81 (Watumiaji waliojiandikisha na kuchangia katika muda wa siku 30 zilizopita)
Bofya hapa kwa kupata namba za sasa
Angalia idadi ya wasomaji kwa makala mbalimbali
(fungua anwani kwa browser yako, badilisha "Mwanzo" kwa jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa)
  • na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani.
(unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)

Jumuia za Wikimedia

Commons
Ghala ya Nyaraka za Picha na Sauti
Meta-Wiki
Uratibu wa Miradi yote ya Wikimedia
Wiktionary-logo.svg
Wikamusi
Kamusi na Tesauri
Wikibooks-logo.png
Wikitabu
Vitabu vya bure na Miongozo ya Kufundishia
Wikiquote-logo-51px.png
Wikidondoo
Mkusanyiko wa Nukuu Huria
Wikisource-logo.png
Wikichanzo (Wikisource)]
Matini za vyanzo asilia kwa Kiswahili
Wikispishi
Kamusi ya Spishi
Graduation cap.png
Wikichuo
Jumuia ya elimu
Wikinews-logo.png
Wikihabari
Habari Huru na Bure