Bomu la nyuklia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mlipuko wa bomu ya kinyuklia ya jaribio huko Nevada (Marekani) mwaka 1951.

Bomu la nyuklia ni silaha inayosababisha mlipuko mkubwa sana. Kati ya silaha zote, hiyo ni yenye nguvu na pia yenye hatari zaidi.

Misingi ya kifizikia[hariri | hariri chanzo]

Nishati ya mlipuko huo yatokana na mmenyuko mfululizo wa kinyuklia ambayo ni ama

Katika mmenyuko wa kinyuklia sehemu ya mada ya atomi hugeuzwa kuwa nishati.

Mabomu ya kawaida hutumia nishati ya mmenyuko wa kikemia ambamo viini atomia havibadiliki.

Aina za mabomu ya nyuklia[hariri | hariri chanzo]

Kutokana na aina mbili za mmenyuko wa kinyuklia kuna aina mbili za silaha zinazoitwa:

Mabomu atomia hutengenezwa kwa kutumia urani au plutoni. Isotopi za elementi hizo zafaa kupasuliwa na kuingia katika hali ya mmenyuko mfululizo.

Mafundi wakimaliza maandalizi ya bomu la Hiroshima mwaka 1945.

Mabomu ya hidrojeni yatumia isotopi za hidrojeni hasa deuteri na triti inayoungana kuwa heli. Mmenyuko huu huanzishwa kwa mlipuko wa bomu atomia ndani ya bomu ya hidrojeni. Nishati ya mabomu ya hidrojeni yapita kiwango cha mabomu atomia mara 100.

Uharibifu[hariri | hariri chanzo]

Kama kila bomu silaha hizi zaleta uharibifu kwa njia ya:

Kutokana na nishati kubwa inayopatikana matokeo yote mawili hushinda silaha za kawaida zinazotumia nishati ya kikemia tu.

Mabomu ya nyuklia zina tokeo la ziada ambalo ni:

Uwezo wa silaha hizi[hariri | hariri chanzo]

Nishati inayopatikana kwa njia ya mmenyuko mfululizo wa kinyuklia ni kubwa sana. Bomu moja la nyuklia yatosha kuharibu kabisa mji jinsi ilivyotokea mwaka 1945 huko Hiroshima na Nagasaki. Mabomu ya 1945 yalikuwa madogo sana kuliko mabomu yaliyotengenezwa baadaye.

Tangu Nagasaki hakuna bomu nyingine lililotumiwa vitani. Milipuko yote iliyofuata ilikuwa ya jaribio tu ama jangwani au baharini pasipo watu. Nchi zote ziliogopa uharibifu mkubwa kupita kiasi, ingawa hasa nchi kubwa za Marekani na Urusi ziliendelea kutengeneza maelfu ya mabomu.

Giza na baridi[hariri | hariri chanzo]

Tangu miaka ya 1980 imejulikana ya kwamba milipuko ya robo hadi nusu ya silaha za nyuklia zilizokuwepo tayari ingetosha kukomesha uhai duniani kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo ingetokea kwa sababu ya kiasi kikubwa cha vumbi kinachorushwa hewani na milipuko hii. Vumbi hiyo ingejaza anga na kuzuia nuru ya jua kufika kwenye uso wa dunia hivyo kusababisha giza pamoja na kushuka kwa halijoto kwa muda wa miaka kadhaa.

Mnururisho[hariri | hariri chanzo]

Hatari nyingine inayojulikana ni mnururisho wa kinyuklia. Imejulikana kutokana na milipuko ya kwanza ya 1945 na majaribio ya baadaye ya kwamba watu na wanyama hufa kutokana na ugonjwa nururifu wakiathiriwa na kiasi kikubwa cha mnururisho au kupata kansa baadaye kwa wingi. Mnururisho huo hukaa kwa muda wa miaka katika ardhi, pia hukusanywa na mimea hasa katika matunda na nafaka. Kwa njia hii yaathiri tena watu wanaotumia mimea hiyo au wanyama waliotumia mimea ile kama chakula.

Imekadiriwa ya kwamba milipuko mingi katika vita atomia ingesababisha kiasi cha mnururisho kitakachobebwa na mawingu na upepo hadi pembe za dunia na kupeleka kifo hata pale pasipo vita.

Nchi zenye silaha za nyuklia
nyekundu – Nchi tano za kwanza zenye silaha za nyuklia zilizopatana kutosambaza teknolojia husika;
njano nyeusi – Nchi nyingine zinazojulikana kuwa nazo;
zambarau – Nchi zilizokuwa nazo zikaziondoa;
buluu - Nchi zinazojulikana zilikuwa na miradi ya utafiti wa silaha hizO zamani lakini bila kutengeneza;
njano – Nchi zinazotuhumiwa kuwa zinaendesha utafiti wa kujenga silaha za nyuklia kwa siri;
zambarau nyeupeKorea ya Kaskazini ilianza kutengengeneza silaha za nyuklia lakini ikapumzisha mradi;

Teknolojia ya kufyatua mabomu ya nyuklia[hariri | hariri chanzo]

Kuna hasa namna mbili za kufikisha mabomu haya panapolengwa:

Kuna pia mabomu madogo yanayoingizwa katika makombora ya mizinga.

Palikuwa pia na mabomu atomia yanayofichwa kama bomu ardhini.

Nchi zenye mabomu ya nyuklia[hariri | hariri chanzo]

Nchi ya kwanza iliyotengeneza mabomu hayo ilikuwa Marekani. Ilifuatwa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia na Umoja wa Kisovyeti, Uingereza na Ufaransa. Baada ya China kuwa na bomu hilo pia tangu mwaka 1964 nchi hizo tano zilijaribu kubana usambazaji wa silaha hizo kwa mkataba wa kimatifa.

Lakini nchi kadhaa ziliendelea kufanya utafiti na kugundua mbinu za kutengeneza silaha hizo kama vile Uhindi (1974) na Pakistan (1998).

Afrika Kusini ilikuwa na silaha za kinyuklia lakini zimebomolewa baada ya mwisho wa apartheid.

Wataalamu wengi huona kuwa Israel ina pia mabomu haya lakini nchi haijawahi kukubali kama zipo.

Korea ya Kaskazini ililipusha bomu ya kwanza ya majaribio mwaka 2006 lakini imetangaza baadaye ya kwamba haitaendelea.

Science.jpg Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bomu la nyuklia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tovuti za Nje[hariri | hariri chanzo]