Uprotestanti
Uprotestanti ni aina ya Ukristo iliyotokana na Kanisa Katoliki huko Ulaya Kaskazini katika karne XVI kufuatana na tapo la kidini na la kisiasa maarufu kwa jina la "Matengenezo ya Kiprotestanti". Wahusika wakuu wa tapo hilo ni Martin Luther na Yohane Kalvini.
Asili ya jina[hariri | hariri chanzo]
Mwaka 1529, kikao cha Bunge la Speyer (Ujerumani) lilikataza tena uenezaji wa Matengenezo katika Dola Takatifu la Kiroma mpaka Mtaguso mkuu utakaporudisha utaratibu ndani ya Kanisa.
Lakini watawala waliomuunga mkono Luther walitoa hati ya pamoja inayoanza na maneno Protestamur, yaani Tunapinga.
Mwaka 1555 Amani ya Augsburg ilipitisha kauli ya kwamba cuius regio, eius religio, yaani kila raia anapaswa kufuata madhehebu ya eneo anamoishi, kadiri ilivyopangwa na mtawala wake, la sivyo ni lazima ahame.
Teolojia[hariri | hariri chanzo]
Uprotestanti unagawanyika katika maelfu ya madhehebu tofauti, lakini inawezekana kutambua mambo kadhaa yanayolingana katika hayo yote:
- kusisitiza Biblia kama msingi wa imani.
- kusisitiza "wokovu kwa njia ya imani".
- kusisitiza ukosefu wa binadamu na haja ya damu ya Yesu kama kafara iliyopangwa na Mungu.
Uenezi[hariri | hariri chanzo]
Leo Waprotestanti wote duniani wanakadiriwa kuwa kati ya 800,000,000 na 1,000,000,000.
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- Cook, Martin L. (1991). The Open Circle: Confessional Method in Theology. Minneapolis, Minn.: Fortress Press. xiv, 130 p. N.B.: Discusses the place of Confessions of Faith in Protestant theology, especially in Lutheranism. ISBN 0-8006-2482-3
- Dillenberger, John, and Claude Welch (1988). Protestant Christianity, Interpreted through Its Development. Second ed. New York: Macmillan Publishing Co. ISBN 0-02-329601-1
- McGrath, Alister E. (2007). Christianity's Dangerous Idea. New York: HarperOne.
- Nash, Arnold S., ed. (1951). Protestant Thought in the Twentieth Century: Whence & Whither? New York: Macmillan Co.
- Noll, Mark A. (2011). Protestantism: A Very Short Introduction. Oxford: Oxford University Press.
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- "Protestantism" from the 1917 Catholic Encyclopedia
- World Council of Churches World body for mainline protestant churches
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uprotestanti kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |