Italia
|
|||
Lugha rasmi | Kiitalia; kijimbo pia Kijerumani, Kifaransa, Kiladino, Kislovenia, Kisardinia | ||
Mji Mkuu | Roma | ||
Rais | Sergio Mattarella | ||
Waziri Mkuu | Paolo Gentiloni | ||
Eneo | 301.338 km² | ||
Wakazi | 60,674,003 (31-7-2015) (23º duniani) | ||
Wakazi kwa km² | 201.7 | ||
JPT | 31,022 US-$ (2008) | ||
Pesa | Euro | ||
Wakati | UTC+1 | ||
Wimbo wa Taifa | Fratelli d'Italia (Ndugu wa Italia) | ||
Sikukuu ya Jamhuri | 2 Juni | ||
Sikukuu ya Taifa | 25 Aprili | ||
Simu ya kimataifa | +39 | ||
Jamhuri ya Italia ni nchi ya Ulaya Kusini. Eneo lake ni km² 301.338 ambalo lina wakazi 60,574,003 (31-7-2015): ni nchi ya 23 duniani kwa wingi wa watu, lakini ya 12 kwa uchumi.
Makao makuu ni jiji la Roma, lenye umuhimu mkubwa katika historia ya dunia nzima.
Yaliyomo
Jiografia[hariri | hariri chanzo]
Umbo lake linafanana na mguu linalozungukwa na maji ya Mediteraneo pande tatu.
Visiwa viwili vikubwa vya Sicilia na Sardinia ni sehemu za Italia pamoja na visiwa vidogovidogo.
Imepakana na Ufaransa, Uswisi, Austria na Slovenia.
Nchi huru mbili ndogo zinazozungukwa na eneo la Italia pande zote ni San Marino na Vatikano.
Mto mrefu zaidi unaitwa Po na una urefu wa kilomita 652. Mito mingine ni Tiber, Arno n.k.
Maziwa makubwa zaidi ni: Garda (km2 367.94), Ziwa Maggiore (212.51, likiingia Uswisi), Ziwa la Como (145.9), Trasimeno (124.29) na Ziwa la Bolsena (113.55).
Mikoa[hariri | hariri chanzo]
Bendera | Jina | Makao makuu | Eneo (km2) | Wakazi | Msongamano wa watu/km² | Wilaya | Miji | Miji mikubwa | Hali ya utawala |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Abruzzo | L'Aquila | 10,763 | 1,307,919 | 122 | 4 | 305 | - | Kawaida | |
Bonde la Aosta | Aosta | 3,263 | 126,933 | 39 | 0 | 74 | - | Kujitawala | |
Apulia | Bari | 19,358 | 4,045,949 | 209 | 6 | 258 | Bari | Kawaida | |
Basilicata | Potenza | 9,995 | 575,902 | 58 | 2 | 131 | - | Kawaida | |
Calabria | Catanzaro | 15,081 | 1,954,403 | 130 | 5 | 409 | Reggio Calabria | Kawaida | |
Campania | Napoli | 13,590 | 5,761,155 | 424 | 5 | 551 | Napoli | Kawaida | |
Emilia-Romagna | Bologna | 22,446 | 4,354,450 | 194 | 9 | 348 | Bologna | Kawaida | |
Friuli-Venezia Giulia | Trieste | 7,858 | 1,219,356 | 155 | 4 | 218 | Trieste | Kujitawala | |
Lazio | Rome | 17,236 | 5,550,459 | 322 | 5 | 378 | Rome | Kawaida | |
Liguria | Genoa | 5,422 | 1,565,349 | 289 | 4 | 235 | Genoa | Kawaida | |
Lombardia | Milan | 23,861 | 9,749,593 | 409 | 12 | 1544 | Milan | Kawaida | |
Marche | Ancona | 9,366 | 1,541,692 | 165 | 5 | 239 | - | Kawaida | |
Molise | Campobasso | 4,438 | 312,394 | 70 | 2 | 136 | - | Kawaida | |
Piemonte | Turin | 25,402 | 4,366,251 | 172 | 8 | 1206 | Turin | Kawaida | |
Sardinia | Cagliari | 24,090 | 1,637,193 | 68 | 8 | 377 | Cagliari | Kujitawala | |
Sisilia | Palermo | 25,711 | 4,994,817 | 194 | 9 | 390 | Catania, Messina, Palermo | Kujitawala | |
Trentino-Alto Adige/Südtirol | Trento | 13,607 | 1,036,707 | 76 | 2 | 333 | - | Kujitawala | |
Toscana | Firenze | 22,994 | 3,679,027 | 160 | 10 | 287 | Firenze | Kawaida | |
Umbria | Perugia | 8,456 | 885,535 | 105 | 2 | 92 | - | Kawaida | |
Veneto | Venisi | 18,399 | 4,865,380 | 264 | 7 | 581 | Venisi | Kawaida |
Historia[hariri | hariri chanzo]
Akiolojia imethibitisha uwepo wa Homo neanderthaliensis miaka 200,000 iliyopita. Homo sapiens sapiens alifika miaka 40,000 iliyopita.
Kufikia milenia ya 1 KK wakazi wengi walikuwa wa jamii ya Kizungu na kutumia lugha za Kihindi-Kiulaya.
Peninsula ya Italia iliunganishwa mara ya kwanza na Jamhuri ya Roma (509-27 KK), lakini hiyo ilipoenea Ulaya kusini na magharibi, Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi ikawa na sura ya kimataifa.
Umoja ulipotea kuanzia uvamizi wa Roma (476 BK) na hasa baada ya ufalme wa Karolo Mkuu.
Juhudi za kuurudisha zilifanywa hasa katika karne ya 19, ambapo Ufalme wa Sardinia uliteka sehemu kubwa ya Italia (hasa miaka 1860, 1866 na 1870).
Baada ya vita vikuu vya pili iligeuka Jamhuri yenye katiba inayotia mamlaka kuu mikononi mwa bunge.
Ni kati ya nchi sita zilizoanzisha Umoja wa Ulaya mwaka 1957 ikaendelea kuunga mkono ustawi wake hadi uanzishaji wa pesa ya pamoja (Euro).
Maendeleo[hariri | hariri chanzo]
Italia ni nchi iliyoendelea, ikiwa na nafasi ya nane kwa nguvu ya kiuchumi duniani, hivyo ni mwanachama wa G7, G8 na G20.
Sanaa na utalii[hariri | hariri chanzo]
Pia ni nchi inayongoza duniani kwa kuwa na mahali pengi (51) pa kimaumbile na pa kihistoria palipoingizwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia".
Kwa sababu hiyo pia inashika nafasi ya 5 kati ya nchi zote zilizo lengo la utalii.
Watu[hariri | hariri chanzo]
Wananchi wana sifa za pekee kati ya Wazungu wote, hata upande wa DNA, kutokana na jiografia na historia ya rasi.
Kutokana na umati wa Waitalia waliohama nchi hiyo karne za nyuma, sasa zaidi ya watu milioni 60 nje ya Italia wana asili ya nchi hiyo, mbali na raia zaidi ya milioni 4 wanaoishi nje.
Lugha rasmi ni Kiitalia, inayotegemea zaidi lahaja za Italia ya Kati, lakini siku hizi inatumiwa na wananchi walio wengi hata katika mikoa mingine, ambayo kwa jumla ni 20.
Upande wa dini, wengi wao (81.2%) ni Wakristo wa Kanisa Katoliki, wakifuatwa na Waorthodoksi (2.5%, wengi wao wakiwa wahamiaji hasa kutoka Romania). Uhamiaji mwingi wa miaka ya mwisho wa karne ya 20 umeleta pia Uislamu (2.6%) na dini nyingine.
Watu maarufu[hariri | hariri chanzo]
- Fransisko wa Asizi
- Marko Polo
- Dante Alighieri
- Katerina wa Siena
- Bernardino wa Siena
- Kristofa Columbus
- Amerigo Vespucci
- Yohane wa Verrazzano
- Nikola Machiavelli
- Leonardo wa Vinci
- Michelangelo
- Raffaello Sanzio
- Karolo Borromeo
- Papa Pius V
- Galileo Galilei
- Amedeo Avogadro
- Alessandro Volta
- Giuseppe Verdi
- Giuseppe Garibaldi
- Yohane Bosco
- Antonio Meucci
- Papa Pius X
- Maria Montessori
- Guglielmo Marconi
- Benito Mussolini
- Enrico Fermi
- Papa Yohane XXIII
- Pio wa Pietrelcina
- Carlo Rubbia
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- (2005) Italy - Eyewitness Travel Guides. DK. ISBN 1-4053-0781-1.
- (2004) Northern Italy - Insight Guides. APA Publications. ISBN 981-234-903-0.
- Hacken, Richard. History of Italy: Primary Documents. EuroDocs: Harold B. Lee Library: Brigham Young University. Iliwekwa mnamo 6 March 2010.
- FastiOnline: A database of archaeological excavations since the year 2000. International Association of Classical Archaeology (AIAC) (2004–2007). Iliwekwa mnamo 6 March 2010.
- Italy History – Italian History Index (Italian, English). European University Institute, The World Wide Web Virtual Library (1995–2010). Iliwekwa mnamo 6 March 2010.
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- Online resources about Italy at UCB Libraries GovPubs
- Italia katika Open Directory Project
- Italian Higher Education for International Students
- Italian National and Regional parks
- Italian tourism official website
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
Nchi za Umoja wa Ulaya | |
---|---|
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufalme wa Muungano | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi |
|
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Italia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
- ↑ The Duomo of Florence | Tripleman. tripleman.com. Iliwekwa mnamo 25 March 2010.
- ↑ Brunelleschi's Dome. Brunelleschi's Dome.com. Iliwekwa mnamo 25 March 2010.
- ↑ St. Peter's Basilica (Basilica di San Pietro) in Rome, Italy. reidsitaly.com.
- ↑ See List of largest church buildings in the world; note that the #3 entry, First Family Church building in Kansas, is now a school education complex.
- ↑ Basilica di San Marco.