G7
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kundi la nchi 7 na Umoja wa Ulaya |
---|
|
Kundi la G7 linaundwa na mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa nchi 7 zilizoendelea sana: Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japani, Ufalme wa Muungano na Marekani ambao wanakutana ili kujadili hasa maswala ya uchumi. Umoja wa Ulaya pia unawakilishwa katika G7.
Nchi hizo zinaongoza kwa utajiri wa kitaifa, zikiwa na 64% ya utajiri wote duniani ($263 trilioni) kadiri ya Credit Suisse Global Wealth Report October 2014.[1]
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
- ↑ (October 2013) Credit Suisse Global Wealth Databook 2013. Credit Suisse.
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |