Wacuba wanajitayarisha na kipindi rasmi cha maombolezi, baada ya kifo cha rais wa zamani na kiongozi wa mapinduzi Fidel Castro. Mdogo wake, Raul, amesema mwili wa Fidel utachomwa moto kwa utashi wa kiongozi huyo. Nenda kwenye makala
Bonyeza hapa kusoma Taarifa ya Habari za Ulimwengu kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW
Kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Cuba Fidel Castro viongozi mbali mbali duniani waliomchukulia kama rafiki na mshirika wametoa salamu za rambirambi wakimsifu. Wacuba walioukimbia utawala wake, wamefurahia usiku kucha.
Ulimwengu leo hii umeamka na simanzi ya kuondokewa na kiongozi mashuhuri, aliyekuwa rais wa Cuba Fidel Castro kiongozi huyo alifariki jana usiku na taarifa hiyo ilitangazwa na nduguye rais Raul Castro
Kiongozi wa muda mrefu wa Cuba Fidel Castro amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90. Mwanamapinduzi huyo ameacha historia yenye mchanganyiko wa maoni.
Ankara imekasirishwa na bunge la Umoja wa Ulaya kwa kuunga mkono usitishwaji wa mazungumzo kuhusu uanachama wake. Msemaji wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel asema vitisho kama hivyo havina faida
Wazima moto wanaendelea kupambana kuuzima moto huo mkali kwa siku ya nne leo katika mji wa Haifa nchini Israel. Maelfu ya watu wameyakimbia makaazi yao.
Serikali ya Algeria imepitisha mswada wa kubana matumizi unaojumuisha kuongezwa kwa kodi na kusimamishwa kwa mishahara ili kukidhi kushuka sana kwa mapato yapatikanayo kutokana na mauzo ya gesi.
Vyombo vya usalama nchini Kenya vinasema watu wenye bunduki waliivamia shule moja na kuanza kufyatua risasi katika mji wa Wajir ulio kaskazini mashariki, karibu na mpaka wa Somalia.
Zaidi ya vyama kumi vya upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimeungana kuanzisha kampeni ya kumshinikiza Rais Joseph Kabila kuondoka baada ya muda wake kukamilika mnamo tarehe 20 Disemba.
Majeshi ya Libya yanasema yanaikaribia ngome ya mwisho wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) katika mji wa Sirte, ikiwa ni kampeni ya kuwang'oa kabisa nchini humo.
Marekani imewasilisha pendekezo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kuiwekea Sudani Kusini vikwazo vya biashara ya silaha kufuatia onyo kuwa nchi hiyo iko katika hatari ya kuingia kwenye mauaji makubwa.
Waandamanaji wamekusanyika nje ya mahakama nchini Afrika Kusini kupinga ubaguzi, ambapo raia wawili weupe wanakabiliwa na mashitaka ya kumshindilia kwa nguvu raia mweusi katika jeneza na kumtishia kumchoma.
Kongamano la vijana kutoka mataifa mbali mbali duniani yakiwemo Colombia, Sudan, Nepal na Tanzania lilioandaliwa na chama cha umoja wa mataifa cha Ujerumani mjini Bonn Ujerumani limekamilika
Karibu mataifa 200 yamekubaliana kutengeneza ndani ya kipindi cha miaka miwili sheria za kuutekeleza mkataba wa kihistoria wa kimataifa uliotiwa saini mwaka wa 2015 ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Mkutano wa UN huko Marrakesh, Morocco unafikia kikomo hii leo huku kukiwa na hofu kuwa lengo la kuzuia mabadiliko ya tabia nchi huenda lisiafikiwe iwapo hakutakuwa na uungwaji mkono kutoka Marekani.
Viongozi wa nchi, biashara na wanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani wamemtaka Rais mteule wa Marekani Donald Trump kutoindoa nchi hiyo katika mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa uliofikiwa Paris.
Serikali ya Kenya imesema kwamba imeamua kuchelewesha kufungwa kwa kambi ya wakimbizi ya Dadaab ambayo inaichukulia kuwa tishio la usalama, baada ya shinikizo la kimataifa la kutaka kuwapa wakimbizi hao muda zaidi
Andy Murray amemwonya Novak Djokovic kuwa yuko tayari kuendeleza udhibiti wake kileleni mwa mchezo wa tennis baada ya Mscotland huyo alikamilisha msimu wake katika nafasi ya kwanza ulimwenguni
Mabingwa watetezi Real Madrid, Barcelona, Manchester City na Juventus ni miongoni mwa timu zinazoweza kujikatia tikiti ya hatua ya 16 za mwisho katika michuano ya wiki hii ya makundi katika Champions League
Tuma Facebook Twitter google+ Whatsapp Tumblr Digg Newsvine
Kiungo http://dw.com/p/2TGly
Juhudi za kuzima moto zinaendelezwa Israel, huku waziri mkuu wake Benjamin Netanyahu akitaja moto huo kama aina mpya ya ugaidi, Serikali na waasi nchini Colombia watiliana saini makubaliano ya amani na maafisa 15 nchini Kenya wasitakiwa kwa ufisadi.
Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com
Kiungo http://dw.com/p/2SSau
Dar es Salaam, jiji kuu la kiuchumi na kibiashara nchini Tanzania, Mohammed Khelef alikutana na vijana wanaoshajiisha na kujihusisha na ujasiriamali jamii kupitia mitandao ya kijamii inayowakutanisha na mamilioni ya wenzao kote duniani
Kiungo http://dw.com/p/2SSbU
Nini nafasi ya mitandao hii kwenye kubadili maisha ya vijana wa Kiafrika na kuwafanya kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha yao? Mjini Nairobi, Mohammed Khelef alikutana na mwanablogu maarufu Robert Alai, na hapa anazungumzia kile ambacho mitandao ya kijamii inamaanisha kwake na kwa jamii ya vijana wa Kenya
Kiungo http://dw.com/p/2SSbX
Mohammed Khelef akutana na vijana wa jijini Nairobi wanaotumia mitandao ya kijamii kuhamasishana katika kilimo salama kwenye maeneo ya mijini kupitia kampeni wanayoiita “Adilisha“
Kiungo http://dw.com/p/2SSbZ
Shirika la Jamii Media ambalo linaendesha mtandao wa kijamii wa Jamii Forum linasimamia hivi sasa mradi wa kufuatilia utekelezaji ahadi za wanasiasa waliochaguliwa kwa kura majimboni kwa kutumia mitandao ya kijamii unaoitwa Tushirikishane
Kiungo http://dw.com/p/2SSbV
Katika mji wa kitalii wa Arusha, kaskazini mwa Tanzania, vijana wanaotokea asasi za kijamii na za kibiashara zinazoyalenga makundi maalum ya kijamii, mitandao ya kijamii imekuwa kila kitu kuhusu maisha yao
Kiungo http://dw.com/p/2Sicr
Mitandao ya kijamii inajenga mtandao baina ya watu na inawaleta karibu zaidi hata wale walio mbali.
Kiungo http://dw.com/p/2SSbW
Mwenzangu Mohammed Khelef amezungumza na George Akilimali, mwanzilishi wa Kampuni ya SmartCore Social Enterprise, inayojihusisha na uwezeshaji wa vijana katika kuifikia teknolojia, jijini Arusha, kaskazini mwa Tanzania, juu ya dhana ya "uchumi wa mitandao ya kijamii".
Kiungo http://dw.com/p/2Sp03
Alama unazowacha mtandaoni ni tafsiri inayoelezea wewe ni nani na watu huenda wakakutafsiri kwa alama hizo.
Bonyeza hapa kupata mukhtasari wa habari muhimu duniani katika video fupi za 'Papo Kwa Papo'