Kupro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Κυπριακή Δημοκρατία (Kigiriki)
Kypriakí Dhimokratía
Kıbrıs Cumhuriyeti (Kituruki)

Jamhuri ya Kupro
Bendera ya Kupro Nembo ya Kupro
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: none
Wimbo wa taifa: Ύμνος εις την Ελευθερίαν
imnos is tin eleftherian
Wimbo la uhuru1
Lokeshen ya Kupro
Mji mkuu Nikosia
35°08′ N 33°28′ E
Mji mkubwa nchini Nikosia
Lugha rasmi Kigiriki, Kituruki
Serikali Jamhuri
[[ Nicos Anastasiades]]
Uhuru
Tarehe
16 Agosti 1960
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
9,251 km² (ya 168)
9
Idadi ya watu
 - 2013 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
1,141,166 (ya 158)
838,897
123.4/km² (ya 82)
Fedha Cyprus Pound (CYP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EET (UTC+2)
EEST (UTC+3)
Intaneti TLD .cy3
Kodi ya simu +357

-

1 Sawa na wimbo la taifa la Ugiriki


Ramani ya Kupro

Kupro (pia: Kuprosi, Kipro, Saiprasi, Cyprus) ni nchi ya kisiwani upande wa mashariki wa bahari ya Mediteranea.

Kijiografia ni sehemu ya Asia, lakini kiutamaduni na kisiasa ni sehemu ya Ulaya.

Mji mkuu ni Nikosia.


Historia[hariri | hariri chanzo]

Kisiwa cha shaba[hariri | hariri chanzo]

Watu waliishi kisiwani huko walau kuanzia milenia ya 10 KK.

Zamani za Kale kisiwa kilikuwa chanzo cha shaba nyingi iliyopatikana katika eneo la Mediteranea ya mashariki. Jina la kikemia la shaba "kupri" linatokana na jina la kisiwa.

Katika Biblia[hariri | hariri chanzo]

Kisiwa kinazungumziwa na Biblia ya Kikristo, kwa namna ya pekee kuhusiana na umisionari wa Mtume Barnaba na wenzie Mtume Paulo na Marko Mwinjili kisiwani huko.

Baada ya uhuru[hariri | hariri chanzo]

Tangu vita ya Kupro ya 1974 kisiwa kimegawiwa, huku maeneo ya kaskazini yakiwa anatawaliwa na Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini isiyotambulika kimataifa.

Pamoja na hayo, Kupro imefaulu kujiunga na Umoja wa Ulaya tarehe 1 Mei 2004.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wakazi walio wengi hutumia lugha ya Kigiriki, wengine Kituruki, ambazo zote mbili ni lugha rasmi. Kwa jumla hao wa kwanza ni Wakristo Waorthodoksi (78% za wakazi wote), hao wa pili ni Waislamu (20%).

Wakristo wengine ni Wakatoliki, Waarmenia na Waanglikana.

Dini ina nafasi kubwa katika maisha ya wananchi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Government
Tourism
Official publications

Anwani ya kijiografia: 35°N 33°E / 35°N 33°E / 35; 33


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufalme wa Muungano | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.


Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kupro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kupro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.