Katanga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Shaba katika Kongo

Shaba ni jimbo la kusini-mashariki katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mji mkuu ni Lubumbashi iliyoitwa Elizabethville hadi 1966. Eneo lake ni 496.871 km² kuna wakazi 4,125,000. Kiswahili kinatumiwa kama lugha rasmi.

Jimbo ni maarufu kwa utajiri wake wa maadini mbalimbali. Hasa mashariki ya jimbo ni sehemu ya Kanda la Shaba linaloenea hadi Zambia. Kati ya madini yake ni kobalti, shaba, stani, radiamu, urani na almasi.

Baada ya uhuru wa Kongo mwaka 1960 jimbo liljitenga na kuwa nchi ya pekee chini ya uraisi wa Moise Tshombe. Jeshi la UM lilimaliza kipindi hiki kwa nguvu ya kijeshi na kurudisha Katanga kuwa sehemu ya Kongo tena hadi Januari 1963. Katika kipindi hiki kifupi waziri mkuu wa Kongo Patrice Lumumba aliuawa katika Katanga.

Kiutawala Katanga inaelekea kupasuliwa katika sehemu nne kufuatana na mipango ya katiba mpya ya Kongo.

Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Katanga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.