Ceuta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ceuta (Hispania)

Ceuta (tamka: the-uta; Kiarabu: سبتة sabta) ni mji wa Kihispania ndani ya eneo la Moroko kwenye pwani la Mediteranea. Ceuta iko karibu na mji wa Tetouan upande wa Moroko. Umbali na Hispania ni 21 km kuvuka mlango wa bahari wa Gibraltar. Pamoja na mji wa Melilla ni sehemu ya Hispania na Umoja wa Ulaya kisiasa , lakini kijiografia ni sehemu ya Afrika. Moroko inadai ni sehemu ya eneo lake la kitaifa.

Ceuta ina wakazi 75.276 katika eneo la 18,5 km².

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ceuta inaaminika imeundwa na Karthago katika karne ya tano KK. Jina la Kigiriki la mji imekuwa "Επτά Αδελφοί" (hepta adelphoí - ndugu saba). Tangu Waroma walichukua utawala wa Afrika ya Kaskazini mji ulijulikana kwa jina la "Septem Fratres" (ndugu saba). Jina hili limeendelea hadi leo mji ukiitwa "sabta" kwa Kiarabu au kwa matamshi ya Kihispania "Ceuta".

Kuanzia karne ya tano BK mji umetawaliwa na Wavandali. Mwaka 710 Waarabu Waislamu walifika wakipita Ceuta kuvamia Hispania. Hadi karne ya 14 mji ulikuwa chini ya watawala Waislamu ama Waarabu au Waberiberi.

Mw. 1415 Wareno waliteka Ceuta wakaitawala hadi 1668. Baada ya vita kati ya Ureno na Hispania mji ulikabidhiwa kwa mfalme wa Hispania.

Tangu mwaka 1668 Ceuta imekuwa sehemu ya Hispania. Ndani ya Hispania imekuwa Mji wa kujitawala (Kihispania: ciudad autónoma) tangu 1995.


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia


Flag of Spain.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ceuta kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.