"Ni jambo la kipekee kuwafundisha wanafunzi kutoka Afrika, najua mie ni mmoja wao, najua uwezo wao wa akili, najiona kama nimevaa viatu vyao, najisikia fahari kuwa pamoja nao na kuwafanikisha kumudu kuendesha magari," anasema mkufunzi huyo. Kwa upande wake mwalimu Victor Boadum anaifahamu vema mitaa ya jiji la Berlin kwani amekuwa akiishi katika jiji hilo tangu mwaka 1979.