Shayiri
Shayiri (Hordeum vulgare) |
||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Shayiri
|
||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Shayiri (Kiarabu شعير) ni ni mmea wa familia ya manyasi katika ngeli ya monokotiledoni. Mbegu au punje za shayiri ni nafaka.
Kihistoria ilikuwa chakula muhimu cha watu lakini siku hizi hulimwa zaidi kama chakula cha wanyama. Hata hivyo inaungwa katika mkate na ni sehemu ya chakula cha kawaida cha watu katika nchi za Ulaya ya Mashariki. Inahitajiwa kwa ajili ya vinywaji mbalimbali kama bia au maji ya shayiri inayopendwa huko Japani.
Kwa jumla shayiri inavumilia chumvi katika ardhi kuliko ngano lakini haivumilii baridi kama aina kadhaa za ngano.
Nafasi | Nchi | Mavuno (kwa t elfu) |
Nafasi | Nchi | Mavuno (kwa t elfu) |
---|---|---|---|---|---|
1 | Urusi | 15.773 | 9 | Marekani | 4.620 |
2 | Kanada | 12.133 | 10 | Hispania | 4.448 |
3 | Ujerumani | 11.722 | 11 | Denmark | 3.730 |
4 | Ufaransa | 10.357 | 12 | Poland | 3.461 |
5 | Ukraine | 9.000 | 13 | China | 3.350 |
6 | Uturuki | 9.000 | 14 | Uajemi | 2.900 |
7 | Australia | 6.640 | 15 | Ucheki | 2.280 |
8 | Uingereza | 5.545 | Dunia | 139.044 |
Yaliyomo
Utangulizi[hariri | hariri chanzo]
Shayiri ni zao la nafaka, linalotokana na nyasi zikuazo kwa mwaka, ‘Hardeum vulgare’ shayiri hutumika hasa kulishia mifugo, huku kiasi kidogo kikitumika kutengenezea vileo. (Bia na vinywaji vingine) na kwenye chakula chenye nguvu. Shayiri hutumika kwenye supu, michemsho na mikate katika nchi mbalimbali kama vile Uskochi, na Africa. Mnamo mwaka 2007 kulingana na takwimu za mazo ya nafaka duniani, shayiri lilikuwa ni zao la nne, kwa wingi wa tani milioni 136, ukichukua kilometa za mra 560,000.
Biolojia, mmea wa shayiri ni miongoni mwa familia ya nyasi. Hujichavusha wenyewe, wenye chremosomeu 14. Ni uzao wa nyasi za porini, Horeum vulgare wa spishi ya spontaneum. Inapatikana kwa wingi kwenye maeneo yenye nyasi na miti midogo, na pia hupatikana hata kwenye maeneo yaliyotumika/haribiwa, pembezoni mwa barabara na mashamba makubwa, mbali na hapo hupatikana kwa nadra sana.
Makazi[hariri | hariri chanzo]
Shayiri-pori huwa na masuke yenye uwezo wa kupasuka; na pindi inapokomaa masuke hupasuka na kusambaa na kusaidia kutanwanyika kwa mbegu. Shayiri inayolimwa mashambani ina masuke yasiyopasuka na kusambaa, na kufanya iwe rahisi kuvuna masuke yaliyokomaa. Aina hii ya shayiri inayopasuka ni matokeo ya kuchanganya uzazi ya shayiri jamii mbili tofauti.
Shayiri zenye na zisizo na maganda: Shayiri zisizo na maganda/zilizowahi ni shayiri zenye maganda ambayo ni rahisi kutoka. Ni mazao ya zamani, lakini sasa yamevuta makini ya viwanda vingi na matumizi yake yameongezeka, hasa kwa kiasi cha kingi cha mashati, hasa kwa nguruwe na kuku. Pia shayiri hii imechunguzwa kama inaweza kutumika yote kama punje nzima na matumizi yake kwenye nusa na makapi.
Historia[hariri | hariri chanzo]
Shayiri ndiyo nafaka ya kwanza kuanza kupandwa huko Mashariki karibu na wakati ambao ngano nayo ilipoanza kutumia. Shayiri pori ilipatikana kuanzia kaskazini mwa Africa mapaka Krete upande wa wa Mashariki, na mpaka Tiet kwa upande wa Mshariki. Ushahidi wa shayiri pori wa mwanzo kabisa ni ule kutoka Epipaleolithic huko Ohalo kusinimwa Bahari ya Galilaya, mabaki yanayokadiriwa kuwa ni kabla ya 1700KK. Shayiri ya kawaida ya mwanzo kabisa ilipatikana huko alevantiz leolithic sites, huko Near East, Syria. Shayiri ililimwa huko kwenye peninsula ya Korea tangu 1500-850KK pamoja na mazao mengine kama mtama, ngano na jamii ya mkunde.
Bia ya shayiri penigne ndiyo kinywaji cha kwanza kuwahi kutengenezwa na watu wa Neolithic. Baadaye shayiri ilitumika kama fedha. Pamoja na ngano, shayiri ikawa chakula kikuu huko Misri, ambako ilitumika kutengenezea mikate na bia. Katika dini hasa jamii za zamani, shayiri ilitumika kama zao kuonyesha haki.
Katika Uingereza ya zamani, mikate ya shayiri ilionekana ikitumiwa na watu wa hali ya chini (wakulima) huku wale walio katika ardhi ya juu hula mazao mengine ya shayiri na si mikate. Viazi vilichukuliwa nafasi yake na shayiri mnamo karne ya 19. Uzalishaji: Shayiri ilikuwa inakuzwa kwenye nchi takribani 100 duniani mwaka 2007. Mnamo mwaka 1974, mavuno ya duni yalikuwa tani 148,818,870 na kisha hapo yamekuwa yakipungua.
Ulimaji[hariri | hariri chanzo]
Mmea wa shayiri huweza kukua sehemu mbali mbali. Hakuna hasa maneo ya joto la kawaida ambako hulimwa kama zao la kiangazi na maeneo ya tropiki ambako hupandwa kwama zao la kipupwe. Hulimwa baada ya siku 1-3. Shayiri hupenda kukua katika hali ya ubaridi, lakini haitishiwi sana na mazingira ya baridi.
Shayiri huvumilia sana udongo wa chumvichumvi kuliko ngano, nah ii huweza kuelezea sababu ya shayiri kulimwa kwa wingi sana huko Mesopotamia kutoka milenia ya pili KK na kuendelea. Lakini shayiri hushindwa kuvumilia baridi kama ilivyo kwa ngano ya kipupwe (Thicum, aestivum), lakini huweza kupandwa kama zao la kipupwe kwenye maeneo yenye joto kama vile Australia. Shayiri huwa na msimu mfupi wa kuku na kuvumilia ukame.
Matumizi[hariri | hariri chanzo]
Kulisha wanyama, nusu ya shayiri inayolimwa Marekani hutumika kulishia mifugo. Shayiri ni chakula cha mifugo kwa maeneo mengi duniani na hasa maeneo mengi ambayo hayawezi kukuza mahindi, hasa kaskazini mwa Ulaya. Hutumika pia huko Canada. Kutengeneza vileo; kiasi kikubwa cha shayiri hutumika kuchemsha pombe, ambapo shayiri huwa chaguo sahihi. Ni viungo muhimu kwenye uzalishaji wa bia na wiski.
Vinywaji vya shayiri visivyo na kilevi, kama vile maji ya shayiri na chai ya shayiri (inayoitwa mugisha huko Japan), hutengenezwa kwa kuchemsha shayiri kwenye maji. Mvinyo wa shayiri kilikuwa ni kilevi cha miaka 1200, na kiliandaliwa kwa kuchemsha shayiri kwenye maji, na kisha huchanganywa na mvinyo na viungo vingine kama limao na sukari viliongezwa. Kufikia mwaka 1800, mvinyo mbali mbali na sukari vilikuwa unatengenezwa kutoka viungo vya kigiriki.
Picha[hariri | hariri chanzo]
- Mifano ya shayiri