Kwa mashabiki wengi wa kandanda ya kimataifa,timu ya taifa inaposhindwa japo kwa mabao 3-0 huwa ni uchungu mwingi sana kwa wananchi. Lakini hebu tafakari kichapo cha mabao 30-0 ? Haya basi, timu ya taifa ya visiwa vya Bahari ya Pacific, ya Micronesia ilichapwa 30-0 na Tahiti katika mechi ya kwanza ya kanda hiyo. Masaibu yao hayakuishia hapo, siku ya jumapili, maji yalizidi unga