Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Angalia Msaada wa kuanzisha makala ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.
Je, wajua...
Kutoka kwenye mkusanyiko wa makala za Wikipedia:
... kwamba Ngorongoro imepokelewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO?
Kuni ni ubao unaotumiwa kama fueli ikichomwa motoni ya kupikia au pia ya kupashia nyumba moto. Kwa kawaida kuni inakusanywa penye miti kwa kutafuta sehemu ziliokauka au kwa kukata miti inayopasuliwa kuwa vipande vya ukubwa unaofaa. Kwa kutumia teknolojia kuna pia kuni inayopitishwa kwenye mashine na kupewa umbo maalumu unaofaa majiko ya kisasa.
Watu wengi duniani kwenye nchi za joto hutumia kuni kwa kupikia chakula na kuchemsha maji ya kuoga au kuosha nguo. Tangu karne ya 19 na hasa 20 watu wengi wamehamia kutumia fueli nyingine kama makaa mawe, gesi na madawa yanayotengenezwa kutokana na mafuta ya petroli au pia umeme.
Lakini hata katika nchi baridi zilizoendelea kuna watu wengi kidogo katika mazingira ya misitu wanaopendelea kuendelea kutumia kuni kama mababu zao. Wengine wanafanya hivyo kwa sababu wana maeneo ya miti au msitu hivyo kuni kwao ni bure; wengine wamefuata majadiliano juu ya ekolojia na wanaona ni bora kimaadili kutumia fueli ya nishati mbadala kuliko fueli ya kisukuku; wengine wameona ya kwamba ubao ni fueli nafuu kama wanakaa karibu na misitu na wana uwezo wa kununua majiko ya kisasa kwa nyumba yao. ►Soma zaidi
Picha nzuri ya wiki
Ng'ombe ni wanyama wakubwa wa jenasi Bos. Spishi ya ng'ombe ina nususpishi au aina nyingi lakini ni spishi moja tu.
Ng'ombe hula manyasi na kutembea kwa vidole viwili. Asili yake ni aina za ng'ombe wa pori waliofugwa kwa sababu ya nyama na maziwa. Katika nchi nyingi anatumiwa pia kama mnyama wa mizigo anayevuta plau au magari.
Wataalamu huamini ya kwamba aina zote za ng'ombe zina asili katika mashariki ya kati mnamo milenia ya 9 KK ambako watu waliwahi kuwafuga nas kutoka hapa ufugaji ng'ombe ulisambaa kote duniani.
Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili
Idadi ya makala: 28,238
Idadi ya kurasa zote: 71,517 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
Kamusi elezo ya Wiki ni kamusi elezo huru iliyo chini ya Shirika Lisilo la Kiserikali la Wikimedia Foundation, ambalo linasimamia miradi mingine mbalimbali ambayo imeorodheshwa hapo chini. Mpaka sasa miradi inayopatikana Kiswahili ni Wikipedia na Wikamusi. Wikitabu imewekwa Kiswahili lakini bado ni tupu. Mengine inapatikana Kiingereza pamoja na lugha tofauti.