Mwanzo
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kamusi Elezo ya Kiswahili
|
Karibu kwenye Wikipedia ya Kiswahili!
Wikipedia ni mradi wa kuandika kamusi elezo kamili na sahihi ya maandishi huru.
Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Angalia Msaada wa kuanzisha makala ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.
|
Je, wajua...
|
Kutoka kwenye mkusanyiko wa makala za Wikipedia:
|
|
|
Makala ya wiki
|
Kontena (Kiing. container ) ni sanduku kubwa la metali -hasa feleji_ ambayo vipimo vyake vimesanifishwa kwa matumizi ya kimataifa. Kontena hutumiwa kutunza na kusafirisha bidhaa za kila aina kwa meli, lori au reli. Kontena ndogo husafirishwa pia kwa ndege.
Kontena zimepunguza sana kiwango cha kazi na gharama kinachohitajika kusafirisha mizigo.
Kontena ya kimsingi ni kontena ya futi 20. Hii inamaanisha ya kwamba urefu wake ni futi 20 (mita 6.058), upana futi 8 (mita 2.438) na kimo cha futi 8.5 (mita 2.591). Aina hii huitwa TEU (= twentyfoot equivalent unit) ni kama kipimo cha kutaja kiasi cha mizigo meli inaweza kubeba au kiasi kinachopokelwa katika mabandari. Kontena inaruhusu kubeba mizigo kutoka mahali hadi mahali kwa kutumia usafiri mbalimbali bila kufungua mzigo tena. Kwa hiyo inawezekana kuchukua mzigo ndani ya kontena kiwandani kwa lori, kuihamisha kwa treni hadi bandarini, kuihamisha kwenye meli na kuisafirisha tena kwa lori na reli kwenye nchi inalyolengwa. ►Soma zaidi
|
|
|
Picha nzuri ya wiki
|
Ng'ombe ni wanyama wakubwa wa jenasi Bos. Spishi ya ng'ombe ina nususpishi au aina nyingi lakini ni spishi moja tu.
Ng'ombe hula manyasi na kutembea kwa vidole viwili. Asili yake ni aina za ng'ombe wa pori waliofugwa kwa sababu ya nyama na maziwa. Katika nchi nyingi anatumiwa pia kama mnyama wa mizigo anayevuta plau au magari.
Wataalamu huamini ya kwamba aina zote za ng'ombe zina asili katika mashariki ya kati mnamo milenia ya 9 KK ambako watu waliwahi kuwafuga nas kutoka hapa ufugaji ng'ombe ulisambaa kote duniani.
|
|
Jumuia za Wikimedia
Kamusi elezo ya Wiki ni kamusi elezo huru iliyo chini ya
Shirika Lisilo la Kiserikali la
Wikimedia Foundation, ambalo linasimamia miradi mingine mbalimbali ambayo imeorodheshwa hapo chini. Mpaka sasa miradi inayopatikana Kiswahili ni Wikipedia na Wikamusi. Wikitabu imewekwa Kiswahili lakini bado ni tupu. Mengine inapatikana Kiingereza pamoja na lugha tofauti.
Wikipedia kwa lugha nyingine
Wikipedia kwa lugha nyingine |
|